Utamaduni               Utamaduni Cultural Association             Utamaduni

Karibu kwetu Utamaduni Denimaka
Shirika la Utamaduni/ Utamaduni kulturforening

Kikundi cha utamaduni kilianzishwa mwaka 1977, wakati wasanii walipokwenda kushirikiana na wakulima na wafundi wa utamaduni sehemu ya Usukuma, Tanzania, Afrika mashariki.

Tangia hapo kikundi hiki kiliendelea kueleweka kiutamaduni wa kiafrika hasa wa kisukuma hapa nchii Denimaka. Sana sana kwa ajili ya michezo na ngoma, nyimbo na mila ya jadi tuliendelea kuwaelewesha mambo hayo kwa wenzetu wadenish. Ushirikiano ulingiza idara mbalimbali na miaka hizi tunayo matawi mengi ya kuwafahamisha ifuatavyo.

Utamaduni Dance TroupeUtamaduni Dance Troupe year 2000

Kikundi hiki cha ngoma unaelewesha vitendo ili waangaliaji waelewe maisha ya waafrika, yasiyo ya vita na njaa peke yake, ila pia ni siku za kazi kawaida na siku za kusherehekea pamoja. Vikundi vinaonyesha vitendo vya kuigiza ngoma za kitanzania, pamoja na nyimbo na sauti nyingi kama kuwina na mziki. Vile vile hadithi na maelezo kuhusu maisha ya wasukuma wanaokaa karibu na ziwa Victoria, Nyanza huko kaskazini na magharibi mwa Tanzania.

Wachezaji 6-12 waafrika na wadenish tunaigiza utamaduni na wakulima wasukuma kwa njia ya kuonyesha na kutumia vifaa, vyombo na mawaazi na mapambo kutoka huko Afrika. Pia tunawakaribisha waangaliaji kuingia kucheza kipindi fulani pamoja na kikundi.

Mara fulani tunapenda kufika walimu wanne kufundisha vitendo, nyimbo na ngoma kwa watoto au vijana wanaopenda kufahamu na wasiyo ogopa kutoa jasho kutumia mwili kwa nguvu pamoja na sauti.
Kutokana na kazi ya kuonyesha na kufundisha utamaduni wa kiafrika, mambo hayo hueneza sana nchii Denimaka nzima, na miaka hii unaweza kuona vikundi 20+, wachezaji wanaopenda ngoma za kiafrika sehemu mbali mbali hapa Denimaka, Swedeni na Norway.

Utamaduni Summercamp

Utamaduni Camp year 1999Mwaka 1983 tulianza kupanga mara ya kwanza workshop vya vikundi vyote.
Utamaduni summercamp ya '83 tulipanga weekend nzima kukutana watu 50 katika sehemu ya msitu, Djursland, Denimaka.

Tangia hapo sifa ya Utamaduni Summercamp ilienea kweli na siku hizi tuko watu mia nne tunapofika msituniwiki nzima kucheza na vifaa vyetu vya kiafrika na vya kidenish na kulala kwenye mahema na kupika vyakula na kula kwa pamoja kiujamaa.

Angalia picha za camp!

Kucheza

Kila mwaka, wakati wa baridi wa kukaa ndani ya nyumba, mwezi wa pili kuna kikundi kimoja kinajiita "Watoto na wengine" wanaokaa kisiwani Fyn, kusini mwa Denimaka wanatukaribisha "Vinter-kucheza" weekend nzima. Hapo kwenye shule kubwa tunacheza na tunaongea, watoto na wazima na vijana, kwa ajili ya kugawana upendo wa kucheza ngoma.

Mail

Mail

Utamaduni
Emmelev kaervej 1
8500 Grenaa
Denmark, Europe
info@utamaduni.dk

Tembelea Mtandao wa Taifa Tanzania

English                   Danish

Soma "UMOJA WA MATAIFA OFISI YA IDARA YA HABARI TAARIFA YA ULIMWENGU JUU YA HAKI ZA BINADAMU UTANGULIZI"

chart.dk